Sunday, October 22, 2017

HABARI Serikali haitajenga viwanda – Waziri Charles Mwijage


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage amesema Serikali haitajenga viwanda kama watu wanavyofikiri bali itaweka mazingira mazuri kwa wawekezaji na makampuni binafsi kujenga viwanda.
                                          Mhe. Charles Mwijage

Waziri Mwijage amesema hayo jana jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya siku ya Haki za Binadamu ya Afrika huku akiwataka vijana Wakitanzania kuwa na uthubutu kwa kujiajiri na sio  kukaa kusubiri ajira.
Tuna tatizo moja sisi Watanzania kuna mentality ya kumsubiri mtu fulani hata mtoto akienda shule kitu kikipungua kuna mtu anasubiriwa, huyu mtu mimi sijawahi kumuona…. Tunaposema ujenzi wa uchumi wa viwanda Serikali haitajenga viwanda itaweka mazingira mazuri kwa sisi kujenga viwanda sisi private sector mimi na wewe“amesema Waziri Mwijage kwenye maadhimisho hayo akihimiza vijana wenye uwezo na ubunifu kujitokeza ili wapate sapoti kutoka serikalini au kwenye mashirika binafsi na sio kusubiri kuajiliwa.
Kwa upande mwingine, Waziri Mwijage amesema watu wengi wanapenda kuajiliwa kwa sababu hawajui watoke vipi.
Watu wengi hawajui tutoke vipi na tatizo moja la kuajiliwa, watu wengi walioajiliwa hata yaani hata ukisema kustaafu miaka 70 atapenda apate kuwepo… Uchumi wa viwanda sio mchezo msikilize mheshimiwa Rais anasema hii ni vita ni vita kweli huwezi kusema hii ni vita halafu unacheza densi, njia ya kutoka pointi ya kwanza ni SIDO, kama unataka kutoka nenda TIC, ukitaka kutoka nenda kwenye mifuko, ukitaka kutoka ukikutana na mimi niulize,“amesema Waziri Mwijage.

No comments:

Post a Comment