Monday, October 23, 2017

HABARI Picha: Mhe. Lowassa amtembelea Mhe. Lissu Hospitali Nairobi

Waziri Mkuu wa zamani na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mhe. Edward Lowassa amemtembelea kumjulia hali Mwanasheria Mkuu wa chama hicho Mhe. Tundu Lissu ambaye anaendelea kupatiwa matibu Nairobi nchini Kenya.
Mhe. Lowassa ameongozana mke wake Mama Regina Lowassa ambapo leo hii walifika hospitalini hapo kumjulia hali Mhe. Lissu



Tangu picha za Lissu kuanza kuonakana pindi watu wanapoenda kumjulia hali, viongozi wa juu na wabunge wamekuwa wakifanya hivyo. Miongoni mwao ni mbunge wa jimbo la Tarime vijijini, Mhe. John Heche na mbuge wa Mbeya Mjini Mhe. Joseph Mbilinyi ambao hivi karibuni wameonekana wakiwa katika picha ya pamoja.

JIUNGE NA NYANYA_KAVU.COM  SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia FacebookTwitter  ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka NYANYA_KAVU.!


No comments:

Post a Comment